40°57′N 112°13′W / 40.95°N 112.21°W
Kisiwa cha Antelope (kwa Kiingereza: Antelope Island) ni kisiwa cha Marekani. Kipo ndani ya Ziwa Kuu la Chumvi (Great Salt Lake) katika Jimbo la Utah. Hili ni ziwa la chumvi kubwa zaidi katika Marekani [1] na ziwa kubwa la maji ya chumvi katika Bara la Amerika [2]. Eneo la kisiwa ni square mile 42 (km2 109).
Kiutawala kisiwa hiki kiko ndani ya Kata ya Davis, katika sehemu ya kusini ya ziwa na kuwa eneo linalostawi wakati ziwa liko katika kiwango cha chini.
Kisiwa cha Antelope huwa na paa, nungunungu, melesi, koyote, linxi mkia-mfupi, kondoo pembe-kubwa, baisani wa Amerika 600 na mamilioni ya ndege wa maji. Baisani alikaribishwa katika kisiwa hiki mwaka wa 1893, na kuwa na kudhibitishwa kuwa eneo la uzalishaji wa baisani kwa makusudi ya kuhifadhi.